Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

KARIBU

Ninayo heshima kubwa kukukaribisha katika tovuti rasmi ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB). Bodi hii imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Sura ya 269, Toleo la Marejeo la Mwaka 2023, ikiwa na mamlaka ya kusajili na kusimamia taaluma za Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Wabunifu wa Ndani (Interior Designers), Wabunifu Mandhari (Landscape Architects), Wabunifu wa Uhifadhi (Conservation Architects), Wabunifu wa Meli (Naval Architects), Wabunifu Samani (Furniture Architects), Wakaguzi Majengo (Building Surveyors), na Wasimamizi wa Ujenzi (Construction Managers) nchini Tanzania. Katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria, Bodi imejikita kuhakikisha kuwa wataalamu wote waliosajiliwa wanazingatia viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma, uadilifu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao. Kadhalika, Bodi inaendelea kuhamasisha ubora wa kitaaluma, kulinda maslahi ya umma na kuchangia katika maendeleo endelevu ya sekta ya ujenzi nchini. Tovuti hii imetengenezwa mahsusi kuwa kituo cha taarifa kwa wataalamu, wadau na umma kwa ujumla. Kupitia tovuti hii, utapata huduma na taarifa muhimu zinazohusiana na usajili, maadili ya taaluma, maendeleo endelevu ya kitaaluma (CPD), miongozo ya kisheria na shughuli nyingine muhimu za Bodi. Natoa mwito kwa wataalamu na wadau wote kutumia vyema jukwaa hili ili kuongeza ushirikiano, uelewa, na ufuatiliaji wa viwango vya kitaaluma katika sekta ya ujenzi. Kwa niaba ya Bodi, napenda kuthibitisha dhamira yetu ya kuendeleza mfumo wa udhibiti wenye uwazi, uwajibikaji na ufanisi, unaolenga kukuza taaluma zenye weledi na kulinda heshima ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania.