Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

Dira na Dhamira

Dira/Maono

Kuwa mdhibiti kinara wa taaluma za Ubunifu  majengo, ukadiriaji majenzi na taaluma zinazohusiana katika kanda.

Dhamira

Kudhibiti taaluma za Ubunifu  majengo, ukadiriaji majenzi na taaluma zinazohusiana kwa njia ya:

  1. kusajili wataalamu,
  2. kutoa mafunzo,
  3. kukuza taaluma,
  4. kufuatilia na kusimamia viwango vya kitaaluma,
  5. na kuhakikisha kulindwa kwa taaluma kwa ajili ya mazingira endelevu ya ujenzi na ulinzi wa umma.

Maadili Muhimu

  1. Uadilifu (Integrity): Tunatoa huduma zetu kwa kiwango cha juu cha maadili, siri, uaminifu na uwazi.
  2. Utaalamu (Professionalism): Tunatekeleza majukumu yetu kwa viwango vya juu vya kitaaluma, maadili na ujuzi.
  3. Uwazi na Uwajibikaji (Transparency and Accountability): Tunatekeleza majukumu yetu kwa uwazi na uwajibikaji kikamilifu kwa matendo yetu.
  4. Haki na Usawa (Impartiality): Tumejizatiti kuwa wa haki, sawa, bila upendeleo, na wa kimsingi katika utoaji wa huduma.
  5. Ushirikiano na Kazi ya Pamoja (Teamwork and Collaboration): Tunaahidi kushirikiana kwa mtandao na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yetu.
  6. Kujali Mteja (Customer Focused): Tumejizatiti kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wateja