Sisi ni nani?
Sisi ni nani?
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imeanzishwa na inaongozwa kwa mujibu wa Cap 269, Toleo Lililorekebishwa la Mwaka 2023 la Sheria za Tanzania.
Bodi ina jukumu la kusajili na kudhibiti mwenendo na utendaji wa kitaaluma wa Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Wabunifu wa Ndani (Interior Designers), Wabunifu wa Mandhari (Landscape Architects), Wataalamu wa Uhifadhi wa Majengo (Conservation Architects), Wabunifu wa Meli (Naval Architects), Wabunifu wa Samani (Furniture Architects), Wakaguzi wa Majengo (Building Surveyors), Wasimamizi wa Ujenzi (Construction Managers), pamoja na taaluma nyingine zinazohusiana na sekta ya mazingira ya ujenzi