Programu ya Mafunzo ya Vitendo ya Usanifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi (AQIP)
Muhtasari wa Programu:
AQIP ni mpango rasmi wa mafunzo ya vitendo unaoratibiwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) kwa wahitimu wa Usanifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi, lengo likiwa ni kutoa ujuzi wa kitaaluma na uzoefu wa kazi katika tasnia ya ujenzi.
Eligibility / Sifa za Kushiriki:
-
Mhitimu wa shahada ya Usanifu Majengo au Ukadiriaji Majenzi.
-
Ajaze fomu ya maombi baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu kwa ukamilifu.
How to Apply / Jinsi ya Kujiunga:
-
Tembelea tovuti ya AQRB: www.aqrb.go.tz
-
Jaza fomu ya maombi mtandaoni ya AQIP baada ya kumaliza shahada yako.
-
Ambatisha vyeti vyako vya elimu, kitambulisho, na barua ya utambulisho/taarifa ya kuhitimu.
Duration / Muda wa Programu:
-
Kipindi cha mafunzo kisichopungua miaka 2.
Faida za Kushiriki:
-
Mafunzo ya vitendo chini ya mtaalamu aliyesajiliwa.
-
Uzoefu wa miradi halisi ya ujenzi.
-
Kuelewa taratibu na viwango vya kitaaluma vya AQRB.
-
Uwezo wa kujiandikisha kama Graduate au Professional baada ya kukidhi vigezo