AQRB WASHIRIKI SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI
AQRB WASHIRIKI SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI
Imewekwa: 05 May, 2025

Bodi ya Usajii Wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imemtangaza Bi. Elizabeth Kapemba kulia kuwa mfanyakazi bora wa AQRB kwa mwaka 2025, baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura nyingi dhidi ya washindani wengine. Uchaguzi wa mfanyakazi bora wa AQRB ulifanyika Mei 1 mwaka huu baada ya kuwashindanisha baadhi ya wafanyakazi kutoka katika idara na vitengo kwa kupigiwa kura na watumishi wote na Mchakato huu Uliratibiwa na uongozi wa TAMICO kisha manejimenti kupitisha baada ya mchakato kukamilika.