Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

Jinsi ya Kujisajili Kwenye AQRB

Bodi inatambua aina mbalimbali za wataalamu na wanafunzi. Usajili unategemea hadhi ya muombaji:

Hadhi

Maelezo ya Usajili

Mwanafunzi / Mhituumu (Graduate)

Kwa mhitimu wa shahada inayotambuliwa katika Ubunifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi au taaluma zinazohusiana. Wanaweza kuanza usajili kama Graduate ili kupata uthibitisho wa kuanza mafunzo ya vitendo-AQIP

Mtaalamu (Professional)

Muombaji lazima awe tayari amesajiliwa kama Graduate na kuwa na uzoefu wa vitendo wa taaluma-AQIP chini ya mtaalamu aliyesajiliwa. Baada ya kuthibitishwa na kufaulu mitihani, atasajiliwa rasmi kama Mtaalamu.

Technician

Kwa wahitimu wa kozi za ufundi zinazotambulika, wanaweza kujisajili kama Technician. Hii inawapa heshima ya kitaaluma na kuwezesha kushiriki kwenye miradi chini ya usimamizi wa mtaalamu.

Draughtsman

Kwa wahitimu wa kozi za uchoraji wa usanifu na mbinu za ujenzi. Usajili huu unasaidia kuzingatia viwango vya kitaaluma na kazi salama za uchoraji na mbinu za ujenzi.

Hatua za Jumla za Usajili

  1. Kukidhi sifa za taaluma kulingana na hadhi.
  2. Kuandaa nyaraka muhimu (vyeti, transcripts, kitambulisho, picha ndogo, uthibitisho wa uzoefu).
  3. Kujaza fomu ya maombi mtandaoni kupitia mfumo rasmi wa AQRB-ORS
  4. Kulipa ada husika.
  5. Kuthibitishwa na kuingizwa kwenye rejista rasmi kulingana na hadhi