Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Ujenzi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

Bodi ilianzishwa mwaka gani?

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ilianzishwa awali mwaka 1972 chini ya Sheria ya Bodi ya mwaka 1972. Uanzishwaji wake rasmi kama chombo cha kisheria cha kusimamia usajili na udhibiti wa taaluma za Usanifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi ulifanyika mwaka 1997 kupitia Sheria Na. 16 ya mwaka 1997.

Sheria hiyo baadaye ilifutwa na kutungwa upya kupitia Sheria Na. 4 ya mwaka 2010, na kwa sasa inatekelezwa chini ya Cap. 269, Revised Edition 2023, ambayo ndiyo msingi wa kisheria unaoongoza mamlaka, majukumu na utendaji wa Bodi nchini Tanzania.